Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benckiha amefanya mapinduzi makubwa Simba - Ahmed Ally

Benchikha Morocco.jpeg Benckiha amefanya mapinduzi makubwa Simba - Ahmed Ally

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa, ndani ya muda mfupi ambao kocha mkuu mpya Abdelhak Benchikha ameingia kwenye, tayari amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kikosi hicho.

Ahmed amesema hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii mara baada ya Benchikha kuisimamia Simba kwenye michezo miwili (dhidi ya Jwaneng Galaxy uliomalizika kwa sare na ule wa Al Ahly ambapo Simba ilipoteza kwa bao 1-0).

"Mwana Mapinduziii. Ndani ya muda mfupi amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kikosi chetu. Fitness imepanda maradufu, ukabaji wa hali ya juu, ufundi umeongezeka kwa wachezaji wetu, kiwango cha mchezaji mmoja mmoja kimepanda, hali ya kujiamini kwa wachezaji imeongezeka, morali iko juu," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live