Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha mgeni rasmi Simba kesho

Benchikha Mdas Benchikha mgeni rasmi Simba kesho

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC kesho watakuwa na pambano lao la Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar na pambano hilo litachezwa katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Benchikha ndiye atakuwa mgeni rasmi kama ambavyo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amemtambulisha.

“Kesho mgeni rasmi ni Benchikha, hii ni mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu, sababu nyingine ni kuleta mabadiliko katika Simba SC ambayo hivi sasa inaweza kucheza dakika 270 bila kuchoka.

“Inawezekana Benchikha mnamchukulia kawaida lakini tulienda Morocco kila mtu anamuhusudu, wachezaji wa Wydad waliacha kupiga picha ya ukumbusho walienda kuomba picha na Benchikha,“ amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live