Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha hana hofu ya kufukuzwa Simba - Mchambuzi

Kocha Mpya Simba Benchikha.jpeg Kocha Abdelhak Benchikha.

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji na mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Ibra Kasuga amesema kuwa Kocha Mkuu mpya wa Klabu ya Simba, Abdelhak Benchikha hana hofu ya kufukuzwa kutokana na wasifu wake.

Ibra amesema hayo baada ya Simba kumtambulisha Benchikha jana kama kocha wao mkuu baada ya kuachana na Robertinho hivi karibuni.

"Kuna level fulani ya makocha hasa kama hawa ambao wana confidence na ambao wamekwishashinda dhidi ya timu kubwa Afrika ni makocha ambao huwa hawahofii kitu, ni makocha ambao huwa wana confidence na wanaamini kile wanachokifanya.

"Kwa sababu leo hii wewe Simba utaniambia nini mimi nimemfunga Al Ahly na nikachukua kombe mbele yake, utaniambia nini klabu kama Club Africain walikuwa na miaka takribani 20 bila kuchukua kombe mimi nikaenda na nikawapa.

"Nyinyi Simba mtaniambia nini? Ni kocha ambaye hana hofu ya kufukuzwa kwa sababu tayari Profile yake ipo pale na ana mafanikio mengi ambayo ana uwezo wa kujitambia," amesema Ibra Kasuga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live