Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha azivutia pumzi Azam, Yanga

Benchikha: Tunautaka Ushindi Kesho Dhidi Ya Wydad Benchikha azivutia pumzi Azam, Yanga

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ameanza mapumziko mafupi akiwa kwao Algeria, lakini amewatumia salamu mastaa wa timu hiyo  kwamba watakuwa na kazi nzito ili kupambana na timu mbili za juu.

Benchikha amesema usajili walioufanya una deni la kwenda kuthibitisha kwa kuirudisha Simba kwenye mbio za ubingwa kuzishusha Azam na Yanga ambazo zipo juu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti akiwa mapumziko, Simba haitakiwi kuendelea kukaa chini ya timu hizo kubwa mbili na mara baada ya wachezaji kurejea kutoka mapumziko mafupi wanatakiwa kufanya maandalizi mazito.

Simba itarudi kambini Januari 25 baada ya kocha huyo kutoa mapumziko mafupi kwa wachezaji wote kurudi makwao kisha kurejea kazini haraka.

“Nimewaambia hakuna mchezaji anayetakiwa kukosa siku ya kwanza ya mazoezi bila sababu ni bora uwahi  kuliko kuchelewa tunatakiwa kuanza kazi ngumu kwa pamoja,” alisema Benchikha na kuongeza;

“Tumewaongeza wachezaji wapya kila mmoja ndani ya timu sasa ana hamu ya kuona malengo ya klabu yanafikiwa nani wa kukamilisha hilo? Ni sisi kwenye timu tuna kazi ngumu lakini inawezekana kama kila mmoja atajitoa kwa asilimia mia moja.

“Simba haitakiwi kuendelea kuwa chini kwenye msimamo tunatakiwa kuwa juu na hili halitawezekana kama tutaendelera kufanya kazi kwa mazingira ya kawaida, tunatakiwa kufanya kazi kwa malengo na kuweka juhudi.”

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa pointi 23. Yanga ina alama 30 na Azam inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 31 licha ya kutofautiana mechi ilizocheza, Azam ikicheza 13, Simba 10 na Yanga 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live