Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha awatega mastaa wapya Simba

Jobe Simba SC Benchikha awatega mastaa wapya Simba

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC Abdellhak Benchikha ni kama amewatega kiaina wachezaji wapya waliosajiliwa kupitia Dirisha Dogo, Wachezaji wengine wakipewa mapumziko ya siku 10 baada ya kutoka kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 iliyofika fainali na kufungwa bao I-0 na Mlandege.

Mastaa wapya waliosajiliwa na Simba SC ni viungo washambuliaji Saleh Karabaka kutoka JKU na Ladack Chasambi (Mtibwa Sugar), Kiungo wa Mkabaji Msenegali Babacar Sarr na Washambuliaji wawili Mgambia Pa Omar Jobe na Muivory Coast Freddy Michael Kouablan aliyeongoza kwa ufungaji huko Zambia akifunga mabao 14 na asisti nne katika mechi 16 za Ligi Kuu nchini humo.

Kocha Benchikha amesema timu hiyo ilihitaji ongezeko na mabadiliko ya wachezaji kwenye Dirisha Dogo, hivyo mastaa waliosajiliwa wanahitaji kuziba moja kwa moja mapengo yaliyokuwepo na kuhakikisha timu inafanya vizuri.

“Tulihitaji mabadiliko na kuongeza watu, waliosajiliwa sasa ni jukumu lao kuonyesha umuhimu wao ndani ya timu. Tunataka kufanya vizuri katika kila michuano tunayoshiriki hivyo kila mchezaji anahitajika kuonyesha kwanini yupo Simba SC,”

“Tunaendelea kujenga timu itakayokuwa na ushindani na kucheza soka la kuvutia, tutakaporejea naamini tutatengeneza kikosi imara zaidi.” amesema Benchikha. Beki na kocha zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wachezaji wapya wamebeba matumaini makubwa hivyo hawapaswi kuwaangusha.

“Mchezaji anaposajiliwa anakuwa anategemewa kufanya makubwa zaidi, hivyo ndivyo ilivyo na kwa hao wa Simba SC wakipata nafasi wanatakiwa kuhakikisha wanaonyesha ubora na faida kikosini. Binafsi siwezi kutoa maoni ya moja kwa moja bali nawapa muda niwaone kwanza,” amesema.

Simba SC inatarajia kuingia kambini Jumatano, Juma Lijalo kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika zitakazoendelea mwezi ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live