Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha avunja ukimya ishu ya Baleke kufungashiwa virago Simba

Balekeee Simbas.jpeg Jean Baleke

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Abdehak Benchikha amevunja ukimya na kuzungumza sababu za Jean Baleke kutimka Msimbazi, huku akisisitiza klabu hiyo inahitaji mshambuliaji mkali zaidi kuliko Mkongomani huyo, japo ameshusha nyota wawili wapya Pa Omary Jobe na Freddy Michael.

Baleke alijiunga na kikosi hicho katika dirisha dogo la msimu uliopita akitokea TP Mazembe kwa mkopo, akiwa miongoni mwa washambuliaji mahiri na msimu huu amefunga mabao manane akiwa nyuma ya kinara Stephane Aziz Ki ya Yanga mwenye 10.

Hata hivyo, bila kutarajiwa nyota huyo alitemwa katika dirisha dogo lililofungwa Januari 15 sambamba na Moses Phiri na Kramo Aubin, jambo lililowashangaza wengi, lakini Benchikha amesema ilikuwa lazima Baleke aondoke kwani si mali ya Simba.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kocha huyo alisema licha ya mchezaji huyo kuwepo Simba kwa mkopo, lakini nafasi ya kusalia ilikuwa ndogo kwa sababu ya kanuni za usajili wa nyota wa kigeni na  hitaji la timu kuwa na mchezaji mkali zaidi wa kufunga mabao.

Kama Baleke angekuwa mzawa angesalia ila idadi ya wachezaji wa kigeni haikumruhusu kuendelea na Simba. Tumefanya usajili bora naamini kwani shida kubwa tuliyo nayo ni kutengeneza nafasi nyingi lakini hatuzitumii ni kwa sababu hakuna mshambuliaji mwenye uwezo wa kumaliza kila anapopata upenyo wa kufunga,” alisema.

Katika dirisha lililofungwa hivi karibuni, Simba imefanya usajili wa wachezaji sita kwani mbali ya Jobe na Michael, pia imevuta jembe jingine la kigeni Babacar Sarr na wazawa Salehe Karabaka kutoka JKU, Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar na Charles Balua. Huenda kikosi cha Simba kikawa na moto  kama washambuliaji hao watahamishia rekodi walizotua nazo kwenye timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live