Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha atua Simba na wasaidizi wake

Benchikha Simbaaa Benchikha atua Simba na wasaidizi wake

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi uongozi wa Simba umewatambulisha makocha wapya watatu ambao watakuwa na kikosi hicho kutimiza majukumu yao kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.

Usiku wa kuamkia Novemba 28 makocha hao wametua Bongo na kupokelewa na viongozi wa Simba wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Imani Kajula.

Benchikha raia wa Algeria, ametua sambamba na wasaidizi wake ambao ni Kocha Msaidizi, Farid Zemit (kulia pichani) na Kocha wa Viungo, Kamal Boudjenane (kushoto pichani).

Timu hiyo ilisitisha mkataba wa Roberto Oliveira Novemba 7 muda mfupi baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.

Siku chache tatu zilizopita, Simba ilitangaza kupata kocha mpya akichukuwa nafasi ya Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ambaye aliondoka klabuni hapo kwa makubaliano ya pande mbili.

Mchezo huo wa ligi ulichezwa Novemba 5 Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2023/24 Simba kupoteza.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba amesema wanaamini makocha hao watafanya kazi kubwa kuongeza ari ya ushindi kwenye mechi zao zote za ushindani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live