Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha atampa changamoto Walid?

Benchikha Morocco.jpeg Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhak Benchikha

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), wametoa Top three ya makocha wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka (CAF COACH OF THE YEAR,2023). kumbuka hiyo ni kwamsimu ulioisha ambao umetamatika rasmi June mwaka huu.

Makocha ambao wameingia TOP 3 ni Walid Regragui (Mwalimu wa Morocco) halafu kuna kocha mkuu wasasa wa @simbasctanzania Abdelhak Benchikha na Alliou Cisse wa Senegal.

Ukitazama waalimu wa vilabu amesalia BENCHIKHA pekee, hii ni kutokana na msimu wake bora sana akiwa na USMA, wengine wote mataifa yamewabeba kwenye hizi tuzo kutokana na Ubora wao,

BENCHIKHA msimu wake wa mwaka na nusu pale USMA amebeba mataji mawili ya AFRIKA (CAF), ambayo ni CAF SUPER CUP, ambalo kamfunga bingwa wa Champions League, AL AHLY kule Saudia ni Baada ya kuichapa @yangasc kwenye Fainali ya CAF Confederation Cup msimu jana.

Hivyo mataji mawili ya Afrika yamemfanya kuwa kocha pekee wa klabu kuingia tatu bora, waliosalia ambaye anaweza kusumbuana nae ni WALID wa Morocco.

Walid Status yake ya kutinga nusu fainali ya Kombe la DUNIA inaweza ikampa ukocha wa mwaka AFRIKA, hili halina ubishi na itakuwa dhulma wasipompa, lakini Benchikha nae heshima yake akipewa haitakuwa gumzo.

UTABIRI WANGU.

1.WALID REGRAGUI

2.ABDELHAK BENCHIKHA

3.ALIOU CISSE

Kama itabadilika basi ni BENCHIKHA anaenda namba moja na Walid anarudi namba mbili. Hapo ndiyo maamuzi yalipo wanangu, Senegal wamefanya makubwa lakini kuwepo tatu bora ni heshima kwake.

We unasemaje? Lete hoja zako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live