Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha ampa ramani Sarr

 Babacar Sarr Dimba.jpeg Benchikha ampa ramani Sarr

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo Babacar Sarr jana usiku alicheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi Jamhuri ya Pemba, lakini kuna mkwara amepigwa mapema.

Kocha Abdelhak Benchikha ametuma salamu kwa kiungo huyo aliyejiunga na Simba akitokea US Monastir akisema hakuna mchezaji mwenye jina kubwa ndani ya kikosi hicho, lakini mtu pekee mwenye thamani ni yule ambaye ataivaa kwa heshima jezi ya Simba sambamba na kuipigania kiukweli klabu hiyo.

Benchikha alisema amefurahia usajili wa Sarr kukamilika na kwamba wameshamkaribisha kwenye kikosi kiungo hiyo ila zile picha alizokuwa anamkaba staa wa Al Nasr, Cristiano Ronaldo hazitakuwa na maana kama atashindwa kuonyesha ubora huo akiwa na Simba.

Benchikha alisema ujumbe huo haupo kwa Sarr peke yake, bali ni kwa kila nyota atakayesajiliwa kwenye kikosi hicho na wale waliopo na kwamba, hakuna mwenye umuhimu kuliko mwingine ndani ya muda atakaofanya kazi.

“Hakuna anayepangwa hapa kwenye timu kwa kuangalia jina lake. Mimi sio kocha wa namna hiyo mwenye ubora wa kuipigania Simba na tukaona kwa vitendo huyo ndiye mchezaji mwenye nafasi kubwa ya kutangulia kupewa nafasi. Huyu Sarr ni mchezaji mzuri lakini lazima aonyeshe juhudi. Kwangu atacheza akiwa na ubora,” alisema kocha huyo.

“Tuna kazi kubwa. Nafurahia kuna mwanga naanza kuuona kwa wachezaji. Tunataka wachezaji wanaojituma muda wote. Kila mchezaji anatakiwa kuipigania jezi ya Simba kwa vitendo wote tutaona hilo. Hatacheza mtu hapa kwa kuangalia huko nyuma alifanya kipi.”

Benchikha alisema bado kuna nafasi chache zinaendelea kutafutiwa watu wapya kwenye dirisha hili la usajili ambapo viongozi wakimaliza watatangazwa.

“Nani amesalia nadhani viongozi wanayafanyia kazi. Kuna watu wawili au watatu wakipatikana nina imani mtatangaziwa mara moja.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: