Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha ajifungia na mastaa Simba

Benchikha Kikao Benchikha ajifungia na mastaa Simba

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Simba jana kilirejea nchini baada ya kumaliza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas huko Ivory Coast huku kocha wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha akiwaweka kikao mastaa wake.

Simba ilimaliza mchezo huo kwa suluhu na sasa inatakiwa kuhakikisha inapata ushindi kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumamosi na kufuzu hatua ya robo fainali ikiwa na pointi nane.

Baada ya kutua, Benchikha amesema kuwa ameshakaa na wachezaji wake na kuwaeleza kuhusu umuhimu wa mchezo huo, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Akizingumza na Mwanaspoti mara baada ya kutua nchini Benchikha alisema kabla ya kurejea hapa nchini amefanya kikao kizito na wachezaji wake akiwataka kuhakikisha wanafanya uamuzi kwa heshima ya Simba kwenye mchezo dhidi ya Galaxy.

“Galaxy sio timu rahisi ni kama jeshi lisilotabirika, hakuna aliyedhani kama ingeifunga Wydad Casablanca nchini Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa makundi, hata hapa Simba rekodi zinaonyesha wamewahi kushtua kwa kushinda hapa, nadhani mashabiki na hata wao wachezaji wanalijua hili na tayari nimeshakaa kikao na wachezaji na kuwakumbusha,” alisema Benchikha.

“Kwenye soka mambo ya kushtua kama haya huwa yanatokea, sitaki historia hii ijirudie hapa chini yangu, nimezungumza nao tukiwa kule ugenini jana (juzi) nadhani kila mtu ataelewa tulizungumza nini.

“Tunatakiwa kujipanga na vita nzito ya mchezo huu, nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao wakiwa vitani ndio kitu pekee tunahitaji kutoka kwao,” alisema kocha huyo raia wa Algeria.

Aidha, Benchikha alisema maandalizi yao kuelekea mechi hiyo yanaanza leo na watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunga mabao mengi kwenye mchezo huu kwa kuwa ushindi ndiyo jambo pekee wanalotaka kwa sasa.

“Ili kushinda tunahitaji kufunga mabao ya kutosha lakini pia kujilinda vizuri lakini kule mbele bado hatujawa imara zaidi tutawaongezea wachezaji mbinu za kutengeneza nafasi na kuzitumia kwenye hizi siku tutakazokuwa kambini.” Kuonyesha msisitizo, kocha huyo hajawapumzisha wachezaji.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: