Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha aitwa kamati ya maadili, mwenyewe ajibu mapigo

Benchikha Kibarua Benchikha aitwa kamati ya maadili

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu Wa Simba sc ameitwa kwenye kamati ya nidhamu ya Simba Sc na anapaswa kujibu juu ya kauli yake aliyoitoa kwenye press anatarajiwa kufanya kikao Baada tu ya mechi za Muungano kutamatika.

Aprili 20/4 Baada ya mchezo wa Watani Wa jadi na Simba kupoteza Kwa Magoli 2-1 kocha alitoa maneno yaliyotafsriwa ayakuwa maneno ya kiuungwana Kwa Wachezaji.

Benchikha alisema; “Toka nimeanza kufundisha mpira sijawahi kufundisha Wachezaji wenye vichwa vigumu kama hawa, CV yangu inashuka Kila siku.”

"Kazi yangu ni kufundisha na kuangalia tatizo liko wapi pale ninaposhindwa kupata matokeo. Kuongea chochote juu ya wachezaji wangu ni haki yangu siwezi kupangiwa chakusema juu ya mwenendo wa timu yangu.

"Siku zote ukweli unakuwaga mgumu kupokelewa au kuambiwa ila Mimi ni kocha mwenye sifa zangu katika ngazi ya soccer hivyo mimi nasubiri kitu gani kamati itaamua juu yangu...

"Nipo tayari kupokea matokeo yeyote sababu upande wangu sioni kama kuna sehemu nimekosea sababu kama mimi ndo mwalimu bado napewa mipaka chakuongea juu ya wachezaji wangu hii sio sawa.

"Bado naipenda timu ya Simba ila sitaweza kuzuia maamuzi yatakayo tolewa na kamati ya nidhamu," amesema Benchikha ambaye zipo tetesi za chini chini kuwa ameandika barua kuomba kufungasha virago vyake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live