Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Usajili bado

Benchikha Morocco.jpeg Benchikha: Usajili bado

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha amekuwa mkali baada ya timu yake kulikosa taji la Mapinduzi lakini akasema wanarudi kujipanga huku akitoa tahadhari ya siku moja ya usajili.   

Simba ilipoteza nafasi ya kuchukua taji la pili msimu huu na la kwanza kwa Benchikha kwa kupoteza kwenye fainali hiyo ya jana kwa bao 1-0 dhidi ya bingwa wa mara mbili mfululizo Mlandege ya Zanzibar. 

Akizungumza baada ya mchezo huo Benchikha alisema hawana namna ziadi ya kuyapokea matokeo hayo lakini akitarajia wachezaji wake kujifunza kwa kucheza kwa umakini na akili kubwa.

Benchikha alisema kuna wakati watalazimika kujilaumu wenyewe kwa kushindwa kutengeneza ushindi wao mapema kwa muda ambao waliukamata mchezo na kutengeneza nafasi za kutosha.

"Nafikiri kwa muda mwingi mchezo ulikuwa upande wetu, tuliwamiliki vizuri lakini kinachoniumiza ni namna tulivyoshindwa kutumia nafasi zetu, ukiacha ile ambayo kipa wetu alifanya makosa sijaona kama kulikuwa na hatari kubwa zaidi," alisema Benchikha

"Tunatakiwa kujifunza kupitia haya mashindano, wakati huu tunakwenda kucheza mechi kubwa na ngumu huko mbele, tunatakiwa kujitathimini kwa pamoja wapi tunatakiwa kuongeza nguvu zaidi ili tuwe imara.

Aidha Benchikha alisema kuwa bado Simba haijafanya kitu kikubwa sana kwenye usajili unaofungwa kesho saa 5:59 usiku na kwamba bado kikosi chake kinahitaji watu wenye akili kubwa ya uamuzi wa mchezo.

"Unaona nafasi tunazotengeneza nani anatakiwa kuweka mpira wavuni ni mimi? Viongozi wangu? Mashabiki wetu? Ni wachezaji wetu pekee ambao wenye jukumu hilo.

"Wachezaji wapya walilokuja wanahitaji muda kidogo lakini Simba inahitaji wachezaji bora zaidi, naangalia muda nasubiri kuona kipi kitatokea kwa muda ambao umesalia tutazungumza na viongozi kuona kipi tutafanya."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live