Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Tatizo la Simba hili hapa

Benchikha 0008 Benchikha: Tatizo la Simba hili hapa

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema kuwa tatizo kubwa la timu yake ni umaliziaji kwenye safu ya ulinzi ambayo imekuwa butu na kushindwa kufunga mabao.

Benchikha amesema amesema kuwa anajitahidi kufanya kila kitu ili kuhakikisha wanatatua tatizo hilo kabla ya kukutana na watani zao Yanga, Aprili 20, katika Dimba la Mkapa.

“Tatizo kubwa ninaloliona ni umaliziaji tu hakuna kingine, kwani nimeangalia hata baadhi ya mechi za ligi na nimegundua udhaifu wa washambuliaji wengi wanaocheza Ligi ya Tanzania wanashindwa kutumia nafasi.

"Tunafanya kila kitu, lakini hatuweki mpira wavuni, hii ni shida, nimeamua kubadilisha kidogo mbinu na mfumo ili kuwarahishia kazi ya kufunga, siku hizi chache ambazo tupo hapa Zanzibar nawafua wachezaji wangu ili wawe makini wanapokuwa mbele ya lango,” amesema Abdelhak Benchikha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live