Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Simba tishio inakuja

Simba Mapinduzi Znz.jpeg Benchikha: Simba tishio inakuja

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JNa Ijumaa, Kocha Mkuu wa Simba Mualgeria Abdelhak Benchikha amehudhuria mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kumalizika kwa mapumziko ya wiki mbili huku akisema "Simba Bora inakuja".

Benchikha aliyetumbulishwa Msimbazi Novemba 24, mwaka jana akichukua nafasi ya Mbrazili Roberto Oliveira 'Robertinho', akiongea na Simba TV amesema anafurahi kurejea mazoezini na sasa anandelea na programu kuhakikisha Simba inakuwa bora.

"Tumerudi. Nafurahi kuwa hapa, kuna wachezaji wapya na wale waliokuwepo pia. Tumeanza jana mazoezi na leo tutafuata programu zetu ili kuwa sawa tayari kwa mechi zijazo za ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa leo nitatoa mawazo kuhusu kinachofuata ndani ya Simba, naamini kinachokuja kitakuwa kizuri kwa mashabiki na wapenzi wote wa soka la Tanzania," amesema Benchikha na kuongeza;

Nawafurahia mashabiki wa Simba na namna wanavyoipenda timu yao, kilicho akilini mwangu ni ushindi tu, nawaza kushinda kila mechi tunayocheza na kufika mbali hata kuchukua ubingwa. Simba bora inakuja."

Benchika tangu ametua Simba ameiongoza kwenye mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika akianza kwa kutoa suluhu mbele ya Jwaneng Galaxy kisha kupoteza kwa kufungwa 1-0, na Wydad Casablanca kabla ya kurudiana na kushinda 2-0.

Pia amewaongoza Wekundu wa Msimbazi hao kwenye mechi mbili za Ligi na kushinda moja dhidi ya Kagera Sugar (3-0), kisha kutoa sare ya mabao 2-2, na KMC lakini pia aliiongoza Simba kwenye mechi sita za Kombe la Mapinduzi na kushinda nne, sare moja na kupoteza moja ikiwa ni mechi ya fainali ya mashindano hayo kwa kuchapwa 1-0 na Mlandege.

Mchezo ujao wa Simba utakuwa muendelezo wa Ligi Kuu ambapo itajitupa uwanjani Februari 17, kucheza na Dodoma Jiji katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Simba hadi sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 baada ya mechi 10, nyuma ya vinara Azam yenye pointi 31 ilizovuna katika michezo 12 na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 30 baada ya mechi 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live