Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Simba hatujaja Misri kufungwa

Benchikha Ataja Faida Waliyonayo Dhidi Ya Jwaneng Kocha Benchikha

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Abdelhak Benchikha amewachimba mkwara wapinzani wake, Al Ahly kuwa kilichoipeleka timu yake nchini Misri ni kutafuta ushindi tu na kwenda hatua ya nusu fainali na si kingine.

Benchikha amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari nchini humo kuelekea mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Ahly utakaopigwa kesho Ijumaa, Cairo.

“Hatujaja kufungwa hapa Misri, tumekuja kushinda, kama tungekuwa tumekuja hapa kufungwa, basi tusingekuja kabisa na hatuhofii chochote, tumejipanga kukabiliana nao Al Ahly, ni mechi ngumu lakini tumejipanga kuwakabili kupata matokeo mazuri," amesema Kocha Abdelhak Benchikha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live