Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Nitarudi Tanzania kuinoa Simba

Benchikha: Tunautaka Ushindi Kesho Dhidi Ya Wydad Abdelhak Benchikha.

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Kocha Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema kuwa ipo siku atarejea tena Tanzania kuja kuinoa Simba Sc licha ya kuvunja mkataba na kuondoka klabuni hapo kutokana na matatizo ya kifamilia.

Benchikha aliyesajiliwa na Simba Novemba 24, 2023 akichukua mikoba ya Robertinho, amevunja mkataba wake na Simba jana Aprili 28, 2024 ikiwa ni siku 156 tu (sawa na miezi 5 na siku 4) alizowatumikia Simba akiwapa Ubingwa wa Ligi ya Muungano.

"Nikiwa hapa Tanzania nimeshangazwa sana na upendo wa Mashabiki wa Klabu ya Simba SC, kumbuka sikuwahi kufanya kazi hapa lakini niliishi kama mwenyeji, kwa maana kila mahala nilipopita niliona upendo kutoka kwao, na hili ndilo linalofanya niseme kuwa ipo siku nitarudi kufanya kazi tena hapa.

“Hata ikitokea sitarudi ninawahakikishia Wanasimba kuwa timu hii ipo moyoni mwangu, nitaendelea kupambania hata nikiwa nyumbani, kwa kuonesha ushirikiano wowote utakaohitajika kutoka kwa viongozi ama wachezaji.”

Abdelhak Benchikha.

Licha ya kudai kuwa anakwenda kumuuguza mkewe, lakini yapo maneno yanayosemwa kuwa Kocha huyo mwenye ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika 2023 ameondoka baada ya kuona mwenendo mbaya wa timu hiyo tofauti na yaliyokuwa matarajio yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live