Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha; Kocha la makombe

BechikaaaA0002 Benchikha; Kocha la makombe

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imemtambulisha kocha mpya wa kikosi hicho cha wekundu wa msimbazi, Abdelhak Benchikha kutoka Algeria.

Benchikha ni kocha la makombe, huyu bwana msimu uliopita alifundisha klabu mbili alianza kwanza kwa kuwafundisha RS Berkane ambayo hakufanikiwa kuvuka nayo hatua ya mtoano kwenda ya makundi na Berkane wakaachana naye, baada ya kuachana naye akaenda kujiunga na klabu ya USM Alger.

Akiwa USM Alger alifanikiwa kwenye ligi kumaliza nafasi zile za juu akiwa mshindi wa kombe la FA na pia akafanikiwa kushinda taji la kombe la shirikisho Afrika akiifunga Yanga kwa Aggregate ya mabao 2-2 huku yeye akifaidika kwa mabao ya ugenini, na baada ya hapo akaenda kucheza African Super Cup dhidi ya Al Ahly na akafanikiwa kuifunga bao 1-0, hiyo inatosha kuonesha namna gani ni kocha wa makombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live