Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Huyu ngoma ni mtu na nusu

Ngoma Simbaaaa Ms.jpeg Fabrice Ngoma

Sat, 6 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha amesema kwa sasa anaanza kufurahia ubora wachezaji ambao wameanza kuelewa kwa haraka falsafa anazotaka ndani ya timu hiyo, lakini akamtaja kiungo Fabrice Ngoma.

Benchikha amesema anatamani wachezaji wa timu hiyo wanaendelea kuimarika kwa haraka kama alivyo Mkongomani Ngoma anavyoendelea kuuamsha ndani ya kikosi hicho.

Kocha huyo mwenye taji la Afrika la Kombe la Shirikisho kuliko kocha yeyote aliyepo nchini, alisema Ngoma hana mambo mengi uwanjani akili yake inaamua mambo kwa utulivu juu ya pasi zake.

"Naona jinsi wachezaji wanaimarika hii imenivutia na kuna wakati niliwahi kusema hawajanifurahisha lakini sasa nabadilisha naona wanaanza kucheza kwa utulivu," amesema Benchikha na kuongeza;

"Muangalie kama Ngoma anacheza kwa utulivu sana hataki mambo mengi anachezesha timu na kutupa ulinzi eneo la chini, wengine nataka wapite njia hii hii."

Benchikha aliyewahi kuzinoa Raja Casablanca ya Morocco na USM Alger ya Algeria pia amezungumzia sababu ya timu hiyo kupata ushindi kipindi cha pili kwa kusema inatokana na yeye bado hajazijua timu nyingi za hapa nchini ambapo dakika 45 za kwanza huzitumia kuwasoma wapinzani kabla ya kutumia kipindi cha pili kuwamaliza.

"Mimi ni kocha mpya hapa Tanzania, sizijui timu nyingi wala wachezaji wao, nafurahi napata msaada kwa wasaidizi wangu wananiambia taarifa nyingi, lakini natakiwa pia kufanya maamuzi.

"Ndio maana napenda kutumia kipindi cha kwanza kuwasoma wapinzani na baada ya hapo kipindi cha pili nakuwa nimeshajua ubora wa wapinzani hapo tunaingia na gia kubwa ndio maana mnaona tunakuwa bora," amesema Benchikha aliyetwaa Kombe la Shirikisho Afrika na Super Cup msimu uliopita akiwa na USM Alger ilizozizidi ujanja Yanga na Al Ahly Misri zilizopo kiundi moja kwa sasa katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live