Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bellingham kuchenji namba kisa Mbappe

Jude Bellingham Real Madrid 2023 24 1698938944 121078 Jude Bellingham

Fri, 16 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo, Jude Bellingham amesema yupo tayari kucheza namba yoyote atakayopangwa na kocha Carlo Ancelotti ili tu ipatikane nafasi ya Kylian Mbappe kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

Los Blancos imeanza msimu wake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta kwenye fainali ya UEFA Super Cup na bingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya anakutana na bingwa wa Europa League. Mbappe alianza kwenye mchezo huo na kufunga bao la pili baada ya lile la kwanza kufungwa na Federico Valverde.

Mbappe, alitua Bernabeu akitokea Paris Saint-Germain kwa uhamisho hutu na kusaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Pauni 12.8 milioni kwa kila msimu. Ilimchukua muda kidogo tu kuonyesha makali yake kwenye timu mpya, akifunga baada ya asisti ya Bellingham.

Mwanzoni, Bellingham alicheza chini kidogo kwenye Namba 10 ili kumruhusu Mbappe kucheza kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kwanza, kabla ya Mfaransa huyo kuhamishiwa pembeni na kiungo wa England kupata nafasi ya kusongea mbele. Bellingham wala hajali kuhusu majukumu mapya.

“Tuna timu yenye muundo mpya,” alisema Bellingham.

“Tumeonyesha tumejipata. Kipindi cha kwanza tulikuwa bado tunajitafuta na kipindi cha pili tulicheza vizuri. Kocha ananiamini na ndiyo maana ananibadilisha kwenye nafasi. Naweza kucheza kiungo ya juu. Chochote kocha atataka nifanye, nitafanya. Sijui kama kila siku nitafunga mabao, lakini naamini nitahusika kwenye ushindi wa timu.

“Kylian Mbappe yupo vizuri. Ana kasi, ana ujuzi mkubwa. Ni mchezaji mzuri kucheza naye. Anafanya kazi kama mwehu kwa ajili ya timu. Alistahili kile alichokifanya.” Katika mchezo huo, Bellingham alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi.

Chanzo: Mwanaspoti