Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bellingham kama Modric

Jude Bellingham La Liga Bellingham kama Modric

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Real Madrid Jude Bellingham amesema tangu alipotua alikuwa akimfuatilia kwa makini Luka Modric baada ya kumtengenezea asisti katika ushindi dhidi ya Girona.

Bellingham alifunga bao na kumtengenezea asisti Joselu katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Girona wikiendi iliyopita katika mechi ya LaLiga.

Kiungo huyo amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Carlo Anceloti kwani mpaka sasa ameshaweka kambani mabao sita katika mechi nane za LaLiga na kuipandisha Madrid kileleni katika msimamo.

Akizungumza baada ya ushindi huo Bellingham alisema: "Nilikuwa namuangalia Modric kila siku kwa muda wa miezi mitatu. Nataka kuwa mbunifu zaidi, lilikuwa bao zuri kwa sababu ilikuwa presha kubwa mwanzoni wakati mechi inaanza. Najisikia vizuri sana, muda wote nakuwa huru, nafurahia soka langu hapa, kila ninapovaa jezi ya Madrid siku zote napambana kadri ya uwezo wangu."

Wakati huo huo kipa wa Madrid Thibaut Courtois alisema Chelsea itajuta baada ya kumuachia Kepa Arrizabalaga katika dirisha la usajili la kiangazi.

kwa sasa Kepa anakipiga Madrid kwa mkopo wa msimu mzima akichukua nafasi ya Courtois baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti na atakuwa nje ya dimba msimu mzima.

Courtois alisema “Nadhani Chelsea imefanya makosa walipomuacha Kepa. Ni kipa mzuri mwenye nguvu. Sina shaka ni miongoni mwa makipa watano bora duniani kwa sasa.

Tangu alipotua Los Blancos Kepa alicheza mechi tano na kuruhusu mabao matano msimu huu huku akisifiwa na mashabiki kwani ameziba pengo la Courtois.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live