Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bellingham ampasua kichwa Guardiola

Pep Jude Bellingham ampasua kichwa Guardiola

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Pep Guardiola amekiri kuumwa kichwa kwa sasa akiwaza namna ya kumdhibiti Jude Bellingham.

Manchester City na Real Madrid kwa mwaka wa tatu sasa, zimepangwa kukutana kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya msimu huu kutakiwa kumenyana kwenye robo fainali ya michuano hiyo.

Lakini, safari hii Man City itakuwa na mtihani mzito mbele ya Bellingham. Alipoulizwa kuhusu staa huyo wa Three Lions, Guardiola alisema: “Madhara yake yamekuwa makubwa.

“Imekuwa timu tofauti kabisa na msimu uliopita. Amekuwa na umuhimu mkubwa kwenye timu, ni lazima tutafute namna ya kuweza kumdhibiti.”

Miamba hiyo ya Ulaya kwa misimu miwili iliyopita ilikutana kwenye hatua ya nusu fainali. Madrid ilikwenda kushinda ubingwa mwaka 2022, wakati Man City ilinyakua ubingwa huo msimu uliopita.

Bellingham ameongeza kitu kwenye kikosi cha Real Madrid, ambapo Mwingereza huyo amefunga mabao 20 katika mechi 31 alizocheza tangu alipojiunga na Los Blancos akitokea Borussia Dortmund mwaka jana.

Mechi ya kwanza itafanyika Santiago Bernabeu, Aprili 9, siku ambayo pia Arsenal itakipiga na Bayern Munich. Mechi ya marudiano itakuwa Aprili 17 uwanjani Etihad. Na mshindi atakwenda kumenyana na ama Arsenal au Bayern kwenye hatua ya nusu fainali.

Vijana wa Guardiola ni mabingwa watetezi, lakini kocha huyo wa Man City anafahamu wazi kwamba timu yake bado haijafika kwenye ubora wa kulinganishwa na mahasimu wao hao wa Hispania.

Real Madrid imeshinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tano kwenye misimu 10 iliyopita.

Chanzo: Mwanaspoti