Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bellingham afichua Aaichomwambia Kane baada ya kukosa Penati

Jude Bellingham England Speaks Harry 782048961 Jude Belligham akimpoza Harry Kane

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jude Bellingham amefichua alichomwambia Harry Kane baada ya England kukosa penalti huku kijana mwenye umri wa miaka 19 akionyesha uwezo wa unahodha.

Bellingham alimwambia Harry Kane kwamba ‘bado anaweza kushinda mchezo’ kwa England baada ya kukosa penati dhidi ya Ufaransa.

Nyota huyo wa Tottenham tayari alikuwa amefunga bao la kwanza kabla ya kupata nafasi ya kuisawazishia England kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Les Bleus.

Kwa bahati mbaya haikuwa hivyo kwani Kane alipaisha penati yake juu ya goli, na kuruhusu timu ya Didier Deschamps kupata ushindi wa 2-1 na kutinga hatua ya nusu fainali.

Mara tu baada ya kukosa penati yake juu ya goli, Kane alionekana kufadhaika kutokana na tukio hilo ila Belligham haraka alimfata kumrudisha mchezoni.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Bellingham alifichua kile alichosema kwa faida ya taifa.

Alisema: “Kama kiongozi wa timu – ambayo yuko na vyombo vya habari, uwanjani na nje ya uwanja, niliona ni muhimu nimuweke tu mchezoni kiakili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live