Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki mpya Yanga SC apewa maelekezo, Gamondi achachamaa

Hersi X Gamondi X Beki Beki mpya Yanga SC apewa maelekezo, Gamondi achachamaa

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amepiga simu moja kwa beki mpya kutoka FC Lupopo Chadrack Boka na kumpa maelekezo mazito kuhusu msimu ujao, Mwanaspoti linajua.

Boka ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga akitokea FC Lupopo msimu ujao ataungana na kikosi hicho kipya kwaajili ya kuanza kazi rasmi katika kambi ya mazoezi ambayo kuna uwezekano mkubwa ikafanyika nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwanaspoti akiwa kwao DR Congo staa huyo anayemng’oa Joyce Lomalisa Yanga, alikiri kuwa kocha alimpigia akimkaribisha kwenye timu lakini kuna taarifa Gamondi alitaka kuzifahamu kuhusu kwake ambazo nyingine ni binafsi na baadhi zinafaa kutoa hadharani.

Alieleza kuwa, kocha huyo aliyeongeza mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, alimuuliza zaidi kuhusu msimu wake uliopita ili kufahamu kwake ulikuwa vipi, lakini pia kumpa maelekezo kuhusu maisha mapya ambayo atakutana nayo hivi karibuni.

“Kocha amenipigia akanikaribisha kwenye timu lakini kuna taarifa alikuwa anataka kuzijua jinsi nilivyocheza msimu uliomalizika,” alisema Boka ambaye Yanga inadaiwa kumhamisha kutoka Lubumbashi kwenda Kinshasa nchini DR Congo ili kumkwepesha na hasira za mashabiki wa timu yake ambao hawajapenda kusikia akiondoka.

“Pia ameniambia anataka nikaonyeshe uwezo mkubwa ndani ya Yanga kwa upande wa beki wa kushoto, ameniambia nijiandae kwa ushindani kwani ubora wangu ndio utakaonipa nafasi kwa kuwa wapo wachezaji wazuri pia wanacheza eneo hilo.

“Akaniambia kuna msaidizi wake atanipigia kunipa programu ya mazoezi kipindi hiki ligi imemalizika na nitatakiwa kuifuata sawa sawa na kama sitafuata nitaanza kazi kwa adhabu,” alisema Boka.

Hata hivyo Boka alifunguka namna alivyojihisi kuongea na kocha huyo kwa mara ya kwanza na jinsi alivyoyapokea maelekezo hayo na kusema kuwa;

“Nimefurahia sana mazungumzo yake yamenifanya nijipange vizuri zaidi kwa kuona kuwa na kwenda kufanya kazi na timu yenye kocha mkubwa anayetaka mafanikio lakini zaidi ameniheshimu kwa kuwasiliana na mimi kwanza.”

“Hii ni kwa mara ya kwanza napata uzoefu wa aina hii, lakini imenipa picha jinsi gani kocha huyu yuko makini na hahitaji mchezaji asiye bora katika kikosi chake ndio maana ameiandalia na programu kabla sijajiunga na timu,”aliongeza mchezaji huyo.

Boka alishasaini mkataba baada tu ya ligi kumalizika na kuna uwezekano mkubwa akaungana na kikosi hicho cha Yanga, kwaajili ya maandalizi ya msimu ambako kuna uwezekano mkubwa wasishiriki michuano ya Kagame inayopigwa Dar es Salaam wikichache zijazo.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 anaechezea mguu wa kushoto pia anauwezo wa kucheza kama winga, ni miongoni mwa wachezaji bora ndio maana kupitia mwanaspoti iliandika kuwa, baada ya mashabiki kujua kuwa beki huyo ataondoka waliandamana mpaka kwa viongozi kugomea kuondoka kwa mchezaji huyo.

THAMANI YAKE

Mwanaspoti linajua katika dili hilo Lupopo iliitaka Yanga iweke mezani Dola 100,000 (takriban Sh260 milioni) ili kununua mkataba wa mchezaji huyo ambao ulibakiza mwaka mmoja.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 iliwahi kuwauzia mastaa Patrick Katalay, Pitchou Kongo na Alou Kiwanuka ambao walitamba kwa miaka kadhaa.

MPOLE, NINJA WAMCHAMBUA

Akizungumza na Mwanaspoti, aliyekuwa beki wa Lubumbashi Sports ya DR Congo, Mtanzania Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliwaambia Yanga kwamba: “Endapo atafanikiwa kusaini Yanga itakuwa imepata beki atayewasaidia kuongeza nguvu safu ya mabeki. Ukiachana na ubora wake wa kupiga krosi anajitolea kwa timu.”

“Wakati tumecheza nao muda wote alikuwa anapambana na ana uwezo wa kuwasababisha timu ifanye makosa ambayo yanawapa faulo.”

Kwa upande wake, mshambuliaji aliye mbioni kuachana na FC Lupopo, George Mpole aliyecheza na Boka alisema kitu kikubwa alichokiona kwake ni nidhamu ya kazi kuanzia mazoezini hadi wakati wa mechi.

“Nikimzungumzia uwanjani kama kweli Yanga itamsajili itakuwa imepata beki ambaye ana uwezo wa kupiga krosi, kukaba na kushambulia. Jamaa ana nguvu na kasi. Nimeona hilo tukiwa tunafanya mazoezi, kwani haogopi kujaribu kufanya majukumu mbalimbali uwanjani.

“Ukabaji wake anakukaba kama vile mnacheza na wapinzani na ndio kitu anachokuwa anakwenda kukifanya wakati wa mechi,” alisema Mpole mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

Katibu Mkuu wa Lupopo, Donat Mulongoy aliliambia Mwanaspoti juu ya mashabiki wao kuwa wakali, lakini akasema klabu yao itazingatia maono yao.

Mulongoy amesema Lupopo itafanya usajili mwingine wa maana kuziba nafasi yake ingawa wanatambua kwamba beki huyo ni mtu wa maana katika kikosi chao.

“Mashabiki wanapenda wachezaji wao hasa wakiwa wanafanya vizuri kuwa wakali kama hivi tunawaelewa. Hapa Lupopo mmoja wa wachezaji wetu bora ni Boka. Kila timu ya hapa inatamani kuwa na beki kama huyu,” amesema Mulongoy.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: