Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki majeruhi aitesa Liverpool

Andy Robertson Injury Beki majeruhi aitesa Liverpool

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool imepata pigo baada ya beki tegemeo, Andy Robertson kupata majeraha akiwa katika mjukumu ya kimataifa.

Beki huyo alishindwa kuendelea na mechi ya kufuzu fainali za Euro 2024 pale Scotland ilipokuwa ikimenyana dhidi ya Hispania baada ya kuteguka bega.

Robertson alipata jeraha hilo katika kipindi cha kwanza kwenye mechi hiyo iliyochezwa Sevilla, Hispania ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Nahodha huyo wa Scotland alipata jeraha alipogongana na kipa wa Hispania, Unai Simon na kufanyiwa matibabu uwanjani, lakini alilazimika kuondoka uwanjani hadi mapumziko baada ya kugundulika ameteguka bega.

Beki huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 29 aliondoka uwanjani huku mkono wake akiwa ameuviringisha katika jezi na nafasi yake ikachukuliwa na Nathan Patterson anayekipiga Everton.

Scotland ingefuzu Euro endapo ingepata sare dhidi ya Hispania, lakini ilipokea kichapo cha mabao 2-0 na kujiweka katika hatari zaidi. Pia vijana wa kocha Steve Clarke wanatazamiwa kumenyana na Ufaransa katika mechi ya kirafiki wiki ijayo.

Jeraha hilo limempa hofu kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kwani wanajiandaa kucheza mechi dabi dhidi watani wao Everton itakayopigwa Oktoba 21.

Iwapo Robertson atakosa mechi hiyo ya Ligi Kuu England, Klopp atalazimika kumpanga Kostas Tsimikas kuziba pengo lake.

Kostas, mchezaji wa kimataifa wa Ugiriki alisaini mkataba wa muda mrefu mwezi uliopita baada ya kujiimarisha zaidi katika safu ya kiungo.

Liverpool kwa sasa iko nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kushinda mechi tano, sare mbili na kufunga mechi moja dhidi ya Tottenham Hitspur.

Chanzo: Mwanaspoti