Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki kisiki arejea Yanga

Ninja Yanga E.jpeg Abdallah Shaibu

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya beki wa kati Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kumaliza mkataba wake wa mkopo Dodoma Jiji, amerejea Yanga na ameanza rasmi mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Avic Town, uliopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Ninja alikuwa aungane na wenzake juzi Jumanne, lakini ilishindikana ambapo timu hiyo ilifanya mazoezi ya gym na jana ilifanya ya uwanjani ambapo ndipo aliungana nao rasmi kuanza kukiwasha, ikijiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayopigwa Manungu, Jumamosi, pia wakianza maandalizi kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi.

Chanzo cha ndani cha uhakika kilisema kurejea kwa Ninja ndani ya kikosi hicho, anaweza akaendelea na timu hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu na pia kama atataka kwenda kwa mkopo kwingine watakaa mezani kujadili ili kulinda maslahi ya mchezaji na kocha wa timu hiyo anataka kumtumia kwenye Kombe la Mapinduzi.

“Ninja aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kabla ya kwenda Dodoma Jiji, ambako mkopo wake ulikuwa unaishia dirisha hili dogo, ndio maana amerejea kwenye kikosi chake ili kuungana na wenzake,” kilisema chanzo ndani ya Yanga.

“Kama itahitajika aende kwa mkopo tena yatafanyika mazungumzo kwani bado ni mchezaji wetu, ila atafanya mazoezi na wenzake timu ikijiandaa na dhidi ya Mtibwa Sugar na Kombe la Mapinduzi.”

Chanzo hicho kilisema Ninja ni beki mzuri na wanaamini akipewa mechi nyingi zitamjengea kujiamini na kumrejesha kwenye makali kama alivyokuwa mwanzo ambapo alikuwa anatumika mara kwa mara.

“Angekuwa beki mbaya asingeweza kupata dili nje kipindi kile ambacho alikwenda kucheza Czech timu ya Daraja la Tatu ya MFK Karvina, hivyo Yanga inamtazama kwa jicho la tatu na isitoshe alisumbuliwa na majeraha kipindi fulani hadi akafanyiwaa upasuaji, hivyo asingeweza kurudi kwa kasi,” kilisema chanzo hicho.

Mwanaspoti lilipomtafuta Ninja alijibu kwa ufupi: Nani kakwambia? niache kwanza nikupigie kesho asubuhi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live