Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki huu ni askari polisi

Arjan De Zeew.jpeg Beki huu sasa ni askari polisi

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa zamani wa Ligi ya England, Arjan de Zeeuw (43),ameweka wazi kuwa hivi sasa yeye ni Polisi ambaye anatumia muda wake mwingi kupambana na uhalifu.

Arjan ambaye anafanya kazi hiyo kwao Uholanzi alicheza katika klabu tano tofauti za England kati ya mwaka 1995 na 2008.

Baada ya kucheza soka kwa miaka 17, aliamua kustaafu mwaka 2009 na hivi sasa badala ya kuwakimbiza washambuliaji anakimbiza wahalifu.

”Hii kazi haina tofauti kubwa sana na soka, inahitaji kujua namna ya kushirikiana na timu, tofauti ni kuwa sasa hivi niko zaidi na magari yenye kasi na bunduki, bado ninahitaji kuwa na kasi, mazoezi ya kwenye soka yananisaidia ninapokimbiza watuhumiwa”

Amewahi kuzichezea klabu mbalimbali zikiwemo Wigan Athletic, Portsmouth na ADO’20. Hivi sasa anaendelea kucheza soka kwenye timu ya Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live