Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Yanga yamemkuta, apigwa faini, afungiwa mechi tatu

Dickson Job Yanga Beki wa Yanga, Dickson Job amefungiwa michezo mitatu

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Kati wa Yanga Dickson Job, amefungiwa mechi tatu na kupigwa Faini ya Shilingi za Kitanzania laki tano (500,000).

Adhabu hiyo imekuja kufuatia Beki huyo kumkanyaga kwenye mbavu mchezaji wa Mbeya City Richardson Ng'ondya katika mchezo wa Yanga dhidi ya Mbeya City uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 5.

Kitendo hiko ni kuhatarisha maisha ya mchezaji mwenzake na adhabu hiyo imekuja kwa uzingativu wa kanuni ya 41:5 (5.3) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Klabu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 11 na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live