Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Yanga mambo moto

Doumbia Mamadou 1140x640 Mamadou Doumbia

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kimo cha beki mpya wa Yanga, Mamadou Doumbia ambaye ameonekana kuwazidi mastaa wote wanao cheza nafasi yake kimewaibua wadau ambao wamefunguka kuwa endapo ataweza kusawazisha makosa ya mipira ya juu langoni mwao basi timu hiyo itakuwa imara zaidi.

Doumbia anaurefu wa 1.88 akiwaacha mastaa aliowakuta ndani ya timu hiyo ambao ni nahodha Bakari, Mwamnyeto ambaye ana 1.82, Yanick Bangala 1.79, Ibrahim Bacca 1.77 na Dickson Job ambaye kimo chake ni 1.71.

Yanga inaongoza Ligi ikiwa imefanikiwa kukusanya pointi 56 baada ya kucheza mechi 21 wameshinda michezo 18, wamefungwa mmoja na kutoka sare mechi mbili huku wakiruhusu mabao 10 kwenye michezo hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa soka walisema Yanga imekamilika kwenye safu yake ya ulinzi na ndio maana imeruhusu mabao machache shida ilkikuwa ni kukosa umakini kwenye mipira ya juu ambayo ndio imeighalimu na kuruhusu mabao hayo.

Beki wa zamani wa Simba, Amri Said 'Stam' alisema Yanga imefanya usajili kulinganba na mahitaji usajili wa beki huyo mpya umezingatia mahitaji kwasababu timu yao haikuwa na uhitaji wa wachezaji wengi wameongeza nguvu muhimu.

"Mabeki waliopo ni wazuri na wamethibitisha hilo kutokana na idadi ndogo ya mabao waliyofungwa shida yao kubwa ilikuwa ni aina ya mabao wamekuiwa wakikosa beki ambaye anaweza kuruka ujio wa huyu kama ataingia kwenye mfumo vizuri utasaidia;

"Anakimo sahihi kama atafanya vizuri kazi yake kikosini atapunguza makosa madogo madogo ambayo yameonekana ndani ya timu hiyo."

Straika wa zamani wa Simba, aliyewahi pia kukipiga Jangwani, Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' alisema kimo na uchezaji ni vitu viwili tofauti anaweza akawa mrefu lakini akakosa msaada kikubwa ni kumpa muda nimemuona kwenye mechi na Rhino Rangers alipewa dakika chache siwezi kuzungumzia ubora wake.

"Yanga ilikuwa inauhitaji wa kusajili beki lakini suala la urefu ni ziada tu ubora ndio unatakiwa kuzungumzwa zaidi japo kimop pia kinachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza makosa benchi la ufundi ndio linatakiwa kuwa na nafasi kubwa ya kuzungumzia usajili huu."

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema beki huyo anaitaji muda zaidi ili aweze kuthibitisha ubora wake alifunguka hayo baada ya kumpa dakika 45 za kwanza tangu asajiliwe na timu hiyo.

"Ni mapema sana kumzungumzia Doumbia kwasababu amepata dakika chache za kucheza na timu ambayo haikuwa kipimo sahihi kwetu hivyo ninampa mechi tano zaidi ili aweze kuthibitisha ubora wake japo ujio wake ndani ya timu umeongeza changamoto ya namba ambayo itaongeza ubora wa kila mchezaji akitaka namba ya kucheza kikosi cha kwanza."

Chanzo: Mwanaspoti