Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Yanga aahidi ushindi Tunisia

Dickson Job Kitasa Mlinzi wa kati wa Yanga, Dickson Job

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga tayari kipo Tunisia na juzi asubuhi kilifanya mazoezi kujiandaa na mechi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, US Monastir, huku beki kisiki wa timu hiyo, Dickson Job, akiahidi kupambana ili kutoka na ushindi ugenini.

Yanga ipo Kundi D ya michuano hiyo ikiwa sambamba na TP Mazembe ya DR Congo, Real Bamako ya Mali na US Monastir, ikiwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kucheza hatua hiyo baada ya kufanya hivyo mwaka 2016 na 2018.

Wachezaji wa timu hiyo chini ya makocha Nasreddine Nabi na Cedric Kaze wapo tayari kwa vita hiyo ya Jumapili na Job kwa niaba ya wenzake alisema wamejiandaa kuwasapraizi Watunisia.

Job aliye roho ya ukuta wa Yanga alisema yeye na wenzake wako tayari kuwaduwaza Monastir kwa kuwapa kipigo kitakachowapa pointi tatu muhimu kundini kabla ya kurejea nyumbani kukabiliana na TP Mazembe mechi ya Februari 19.

Alisema kila mchezaji ana morali kubwa kuelekea mchezo huo wakijua kuwa wanipambania Yanga lakini nchi pia kwani mafanikio ya timu hiyo ni furaha ya Tanzania.

“Sisi kama wachezaji tuko tayari kwa asilimia 100 kuipambania timu na nchi na nikiamini kabisa kuwa tunakwenda kufanya vizuri katika mchezo huo.

“Hatuna hofu wala wasiwasi,tutaingia kucheza mchezo huo kama mingine yote tukiaminia tunahitaji ushindi wa kwanza katika hatua hii ugenini, niseme tuko tayari kwa mechi,” alisema Job.

Yanga ilifuzu makundi ya michuano hiyo baada ya kutupwa kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika na kucheza play-off na kuifunga Club Africain ya Tunisia kwa bao 1-0 ugenini, awali ilitoka suluhu nyumbani mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live