Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Yanga: Rivers United ijiandae kwa kichapo

Rivers Pic Data Beki Yanga: Rivers United ijiandae kwa kichapo

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema wamejipanga kuupiga  mwingi dhidi ya Rivers United, mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, Septemba 12 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ninja amesema wana faida ya kuanzia mechi hiyo Uwanja wa Benjamin Mkapa ni kupata ushindi mnono utakaopunguza kazi ngumu mechi ya ugenini. "Tumejipanga kupambania ubingwa mnono, kwani kuna faida ya kuanzia mechi nyumbani, ingawa haimanishi kwamba ni kazi rahisi, ila aridhi yetu haiwezi kutukana,"amesema na ameongeza kuwa;

"Tunatamani kufika mbali kwenye michuano hiyo, kikubwa ni mashabiki wetu tuendelee kushikamana kwa lengo la kufanya vitu vyenye nguvu kwa pamoja,"amesema. Amesema wanaendelea kuhamasishana na kuzingatia mbinu wanazopewa na kocha Nasreddine Nabi. "Tunaendelea kupikwa kisawasawa kiakili na kupewa mbinu za kuupata ushindi mnono kwenye mechi hiyo, kikubwa tunaomba uzima,"amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz