Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Wydad afunguka 'Kutetema' kama Mayele

Wydad Nyieee Beki Wydad afunguka 'Kutetema' kama Mayele

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Simba Sc, Beki wa Wydad AC, raia wa Congo Arsene Zola amefunguka baada ya kuonekana akishangilia kwa staili ya "Kutetema" kama Mayele Fiston baada ya timu yake kupata bao la kwanza kupitia kwa Sambou Bouly.

Arsene alisema kuwa anafahamu ushindani uliopo kati ya Simba Sc na Yanga kupitia kwa wachezaji wenzake ambao pia ni raia wa Congo ndio sababu ya Kushangilia kwa style ya Mshambuliaji wa Yanga raia wa Congo Fiston Mayele.

Wydad ilishinda katika mchezo huo kwa bao 1-0 lakini katika matokeo ya jumla ilikuwa bao 1-1 hali iliyopelekea tinu hizo kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba waliondolewa kwa kufungwa penati 4-3, na kuifanya Wydad kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live