Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Ureno nje miezi miwili

Beki Out Beki Ureno nje miezi miwili

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Ureno Nuno Mendes atakuwa nje kwa miezi miwili ijayo baada ya kuumia paja kwenye mchezo wao wa Kombe la Dunia ambapo timu yake ilikuwa ikiumana dhidi ya Uruguay.

Mechi hiyo iliisha kwa Ureno kuitwanga Uruguay mabao 2-0, na kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora kwenye michuano hii ya Kombe la Dunia .

Ripoti zinasema kuwa Nuno atasalia na timu hadi mwisho wa Kombe la Dunia kwani madaktari wa PSG watamtembelea Qatar hataweza kucheza michezo yote iliyosalia ya Kombe la Dunia, na atakuwa nje hadi Januari 2023.

Mendes mwenye umri wa miaka 20 amekuwa na kiwango bora kabisa katika michuano hii amepata jeraha la paja na hataweza kupona kwa haraka hivyo timu ya Ureno imeamua kumuondoa kwenye kikosi moja kwa moja ili akafanyiwe matibabu.

Mechi ya mwisho ya Ureno watacheza dhidi ya Korea Kaskazini ambapo timu hiyo ya Son Heung min ndio watakuwa wakihitaji sana kupata matokeo ili waweze kufuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano hii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live