Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki United, apata shida ya Kupumua

Victor Lindelof Mlinzi wa Man United Victor Lindelof

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa Manchester United, Victor Lindelof anafanyiwa vipimo baada ya kulalamika kupata shida ya kupumua, ambayo klabu inaripoti kuwa haihusiani na covid19.

Lindelof alibadilishwa na Eric Bailly kwenye mechi ambayo United walishinda dhidi ya Norwich Jumapili, baada ya kulalamika kupata matatizo ya kifua.

Man United pia walijikuta akipata majibu ya maofisa wao kuwa na maambukizi ya Covid19 baada ya kutoka Carrow Road, huku mechi dhidi ya Brentford ikilazimika kuahirishwa.

United, wameweka wazi kuwa suala la Lindelof halihusiani kabisa na maambukizi ya Corona, na anaendelea vizuri. Isipokua taratibu za kitabibu zaidi zinaendelea.

“Victor kwa sasa anaendelea na ratiba ya hatua za uchunguzi. Hata hivyo, ameweza kuendelea vyema ukifananisha na hali aliyokuwa nayo awali kwenye mechi dhidi ya Norwich. Dalili zote zinaonesha hakuna uhusiano na mlipuko wa covid kwenye timu.” -maelezo ya timu juu ya hali ya Lindelof.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live