Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Simba, Azam anyoa rasta, kisa kusingiziwa teja

Said Morad Beki Simba, Azam anyoa rasta, kisa kusingiziwa teja

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Omba Mungu yasikukute kama yaliyomkuta beki wa zamani wa Azam FC na Simba, Said Morad, aliyesingiziwa mambo mazito yaliyofanya abadili muonekano, ili kulinda usalama wake.

Beki huyo aliyekuwa akifunga rasta kichwani, amesema baada ya kupitia maisha magumu yaliyofanya ayumbe kiuchumi, mambo yakabadilika kabisa hadi kufikia baadhi ya watu waliokuwa wakimzunguka kuona ni mtumiaji wa dawa za kulevya.

Ameyasema hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi kuhusu muonekano wake mpya wa kutokuwa na rasta kichwa.

"Nimepitia mambo mengi sana ikiwamo kuyumba kiuchumi, mengine siwezi kuyaweka wazi, sasa nilikuwa nashindwa kuzihudumia rasta zangu kama ilivyokuwa mwanzo hapo ndipo yakaanza kuzuka mambo mengi kwenye jamii," amesema na kuongeza;

"Nikawa nasikia maneno huyo jamaa atakuwa anatumia madawa ya kulevya ndio maana anaonekana kachoka, ikanibidi nizinyoe ili niwe na muonekano ambao hautakuwa wa gharama kubwa ila smati."

Amesema changamoto katika maisha ni za kawaida, kwani kwa sasa anacheza mechi za mtaani (ndondo), huku akipiga mishe za kuuza spea za magari kwenye duka la Juma Shine, lililopo Ilala, Dar es Salaam.

"Naamini kwenye kupambana, mimi bado ni kijana, kila kitu kitakwenda sawa hii ni hali ya kupita tu na najifunza mengi kujua washikaji wa kweli na wale ambao wanakupenda wakati una kitu," amesema

Chanzo: Mwanaspoti