Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibaly amesema kutokuwepo kwa Mane kwenye timu ya taifa sio tatizo kwani bado staa huyo anawapa nguvu wachezaji wenzake.
Saido Mane ambaye alipata majeraha katika mchezo wa Bundesliga ambapo alikua akiitumikia klabu yake ya Bayern Munich na kumsabisha kukosa fainali za kombe la dunia nchini Qatar.
Koulibaly amesema licha Mane kukukosekana katika kikosi hicho bado mtoa hamasa mkubwa na nguvu kwenye timu hiyo kutokana na ukaribu ambao amekua anao na kambi ya timu ya taifa ya Senegal wakati huu michuano ikiendelea nchini Qatar.
Senegal ambao walipoteza mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi kwa mabao mawili kwa bila waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya wenyeji Qatar siku ya Ijumaa.
Kolibaly aliendelea kusisitiza umuhimu wa Mne kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal na kueleza wanajua umuhimu wake hivo wanaamini ataendlea kujumuika nao kwa karibu ili kuendelea kuwapa nguvu.