Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Polisi: Simba inanitaka

Moby Pic Data Beki Polisi: Simba inanitaka

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Saddam SadickMore by this Author BEKI wa Polisi Tanzania, Iddy Moby amesema mchezo wao dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu kutokana na timu zote kuwa katika kiwango bora, lakini akitamba kuwa lazima wapinzani waumie. Lakini akadai kwamba eti Simba wanamtaka.

Azam haijapata ushindi kwa muda mrefu tangu ilipoilaza Dodoma FC mabao 3-0 Novemba 6 kwenye Ligi Kuu na kesho watakuwa ugenini kuwakabili maafande hao wakisaka alama tatu ili kurudisha ari na morali kikosini.

Mobby alisema mchezo huo hautakuwa rahisi licha ya wapinzani kutoka kushinda mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Magereza, lakini hata Polisi Tanzania wamejipanga vizuri.

Alisema wanahitaji kumaliza vyema mwaka kwa ushindi ili wanapouanza mwaka mpya wawe katika nafasi nzuri na kwamba watakuwa makini kuwakabili wapinzani hao.

“Mchezo utakuwa mgumu na mzuri kwa timu zote kutokana na ubora wao, sisi tumejipanga kwa sababu malengo yetu ni kuona tunamaliza ligi katika nafasi nzuri hivyo tunataka ushindi,” alisema Mobby.

Hata hivyo, beki huyo alidai kusakwa na Simba na kuweka wazi kuwa mazungumzo yanaendelea chini ya msimamizi wake na kwamba mambo yakikamilika ataweka wazi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz