Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Orlando Pirates akimbizwa Hospitali

Mako Hospital Paseka Mako akitolewa Uwanjani na gari la wagonjwa

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Orlando Pirates, Paseka Mako alikimbizwa Hospitali kupewa huduma jana Aprili 12 baada ya kupata majeraha walipogongana na kipa Richard Ofori kwenye mchezo wa DStv Premiership dhidi ya Baroka FC uliochezwa Uwanja wa Peter Mokaba.

Ilikuwa ni kwenye muda wa nyongeza ambapo beki huyo aliweza kugongana na mchezaji mwenzake ambaye ni kipa Ofori aliyekuwa akitimiza majukumu yake kuweza kuhakikisha kwamba mpira haujazama kwenye nyavu zake.

Imethibitishwa kwamba kwa sasa beki huyo anapambania afya yake baada ya kupata maumivu ya kichwa na haraka sana mwamuzi wa kati Masixole Bambiso ambaye alikuwa karibu kwenye mchezo huo aliwaita watu wa huduma ya kwanza.

Ofori naye aliweza kutazamwa na kupewa huduma ya kwanza na yote yalifanywa kwa haraka ili kuweza kuokoa maisha ya wachezaji hao waliokuwa wakitimiza majukumu yao.

Kutokana na jambo hilo wachezaji wa timu zote mbili Pirates na Baroka waliunda duara ili kuweza kumlinda mchezaji huyo wakati akipewa huduma ya kwanza kwenye mchezo huo uliokamilika kwa sare ya bila kufugana.

Orlando Pirates wanatarajiwa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali dhidi ya Simba, Aprili 17, Uwanja wa Mkapa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live