Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Mtanzania atua Salford City ya England

Haji Mnogaaa Beki wa kimataifa wa Tanzania, Haji Mnoga

Sat, 31 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kimataifa wa Tanzania, Haji Mnoga jana usiku alikamilisha uhamisho wa kujiunga na Salford City inayoshiriki Ligi Daraja la Nne England.

Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya beki wa kulia, anajiunga na Salford City akitokea Portsmouth ambaye alikulia na kuicheze tangu utotoni.

Mnoga amejiunga na Salford City kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezeka ikiwa mchezaji huyo ataonyesha kiwango bora.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22, alisema kuwa amefurahia kujiunga na Salford City akiamini itamsaidia kupandisha daraja lake.

“Ninajisikia vizuri kwa hili. Lilikuwa ni dirisha refu na nina furaha hili kukaa kwenye mstari kwa sasa na nimeridhika kwa hili kufanyika.

“Ninategemea huu kuwa na mafanikio kwangu. Mara ya mwisho nilipokuja hapa mambo hayakwenda vizuri kama nilivyotegemea. Ninategemea kuanza tena na kufanya vizuri.

“Nimekuwa na mazungumzo vizuri na meneja. Amesema amefurahishwa kufanya kazi na mimi, nami nina shauku ya kufanya kazi na yeye. Anaonekana ni meneja ambaye anaweza kunisukuma na kupata kilicho bora kwangu.

“Ninaweza kusema nitaleta kasi na nguvu. Mimi ni beki ninayependa kujilinda na napenda kucheza pia na napenda kwenda mbele na kusaidia mashambulizi,” alisema Mnoga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live