Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Marumo: Mayele sio mtu wa kawaida

Beki Marumo GG Beki Marumo: Mayele sio mtu wa kawaida

Sun, 21 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yule beki aliyekimbizwa na mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele wakati anatengeneza bao la pili bado anakosa majibu kila akimtafakari Mkongomani huyo na ameishia kusema yule sio mchezaji wa kawaida.

Tshepo Gumede beki wa Marumo Gallants ambaye Mayele alimfanyia ukatili mkubwa akimuwekea mpira mbele kisha kuanza kumkimbiza na akampita na kuwahi mpira licha ya beki huyo kuwa mbele yake kabla ya kuanza mbio hizo.

Haikuwa kukimbiza pekee Mayele akaenda kutoa pasi ya maana akimlipa Kennedy Musonda ambaye naye alimtengenezea bao la kwanza kisha Mzambia huyo akafunga kikatili bao ambalo liliwapa ushindi Yanga ugenini wakitinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Gumede amezungumza na Mwanaspoti jana Jijini hapa akisema bado haamini kama Mayele ana nguvu na kasi za kawaida kwa jinsi alivyomtoka kwenye tukio lile ambapo hakudhani kama anaweza kuwa na mbio za kiasi kile.

Gumede alisema; "Tulikuwa na taarifa za kila aina juu ya ubora wake ndio maana uliona ule mchezo wa kule Tanzania hakufanikiwa kufunga japo alitoa pasi ya bao la pili lakini huku alichofanya bado nakosa majibu sahihi ya ubora wake halisi."

"Tulidhani ana nguvu pekee ndio maana ukaona alipokuwa nyuma yangu nilidhani hataweza kuja kufanya alichofanya lakini kumbe ana kasi kubwa pia, sio rahisi kwa mchezaji mwingine kuwa na kasi ya namna ile.

"Nilitamani kumvuta lakini nikagundua naweza kupewa kadi nyekundu kwa kuwa nilikuwa mtu wa mwisho na alipokaa mbele yangu sikuwa na la kufanya tena,"aliongeza beki huyo aliyegeuka gumzo kwa mashabiki wa Yanga.

Aidha Gumede aliongeza kuwa wala hashangazwi kusikia taarifa kuwa Mayele anaongoza kwa ufungaji kwa ligi ya Tanzania wala Afrika kwa kuwa aina ya mshambuliaji huyo wako wachache duniani.

"Unaona ubora wa Christiano Ronaldo ni kama huyu (Mayele) anajua kufunga na ana kasi, mshambuliaji wa namna hiyo ni rahisi kufanikiwa na kuwa Bora kwa kuwa wanajua kwamba mabeki wengi hawana kasi na huwa tunakutana na wakati mgumu kukabiliana na mshambuliaji wa namna hiyo.

"Kwangu Mimi nawapongeza Yanga kwa kushinda lakini nawaona wanaweza kuwa watu bora kuchukua hili kombe mbele ya USM Alger, tumecheza nao wale tunawajua."

MAYELE ALITAKA KUWAONYESHA

Mayele amesema ili kuonyesha kwamba yeye ni mchezaji mkubwa ilibidi aendeleze kufanya vizuri katika mashindano makubwa.

“Hapa ndani kila mmoja ananijua Mayele lakini nje kulikuwa anayenijua, siku zote mchezaji mkubwa ni yule anayefanya vizuri kwenye mechi kubwa,” alisema Mayele.

Mayele ambaye ndio kinara wa mabao ambaye amebaki kwenye fainali baada ya Chivaviro wa Marumo Gallants kutolewa, alikipotezea kiatu cha mfungaji bora na kuonyesha wazi anahitaji ubingwa.

“kuchukua kiatu huku ubingwa ukiukosa hakutokuwa na maana hivyo nitahakikisha naipigania timu yangu kuchukua ubingwa na mengine yatafuata.”

Chanzo: Mwanaspoti