Sat, 14 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Beki wa kushoto wa Manchester City Benjamin Mendy amekutwa hana hatia katika makosa saba, sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kijinsia yaliyokuwa yakimkabili.
Mahakama haikuweza kupata ushahidi wowote katika kesi yoyote ilotolewa maamuzi jana Januari 13 dhidi ya Mendy.
Hata hivyo bado kuna mashtaka mawili ambayo uchunguzi wake umesemekana bado haujakamilika.
Benjamin Mendy amewekwa pembeni na klabu yake ya Man City ili kushughulika na kesi hiyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live