Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Man Utd aipa ubingwa Arsenal 2023/24

Arteta With Gary Neville Beki Man Utd aipa ubingwa Arsenal 2023/24

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Gwiji na Mchambuzi wa soka, Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Garry Neville amesema kwake yeye Arsenal ina nafasi kubwa ya kuchukua taji la Premier League msimu huu 2023/24.

Sababu kubwa ya Neville kuamini Arsenal itachukua ubingwa ni kutokana na msimu uliopita kuonesha jitihada kubwa za kupambania ubingwa na kuanza vizuri msimu huu.

Mchambuzi huyo wa Sky Sports ambaye enzi zake alikuwa akikipiga beki wa kulia alisema Manchester City ni kama wameridhika na treble waliyochukua msimu uliopita huku pia Arsenal wakifanikiwa kubeba alama tatu dhidi yao tofauti na msimu uliopita.

“Msimu huu tayari Arsenal wamechukua pointi tatu, hatujui huko mbeleni itakuwaje. Nawaona wakiwa mabingwa nafasi hiyo wanayo. City kama wameshiba mafanikio,” alisema Neville ambaye alikiwasha Man United kuanzia mwaka 1992 hadi 2011, akicheza jumla ya mechi 400 na alifunga mabao matano tu.

Chanzo: Dar24