Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Man United aishabikia Nigeria AFCON

Rio Ferdinand Nigeria Beki Man United aishabikia Nigeria AFCON

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa beki wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa Uingereza Rio Ferdinand ambaye kwasasa ni mchambuzi wa vipindi vya televisheni ameweka wazi kuishabikia timu ya taifa ya Nigeria kwenye fainali za kombe la mataifa ya Afrika (Afcon 2023) ambayo imefikia hatua ya fainali itakayowakutanisha Nigeria na Ivory Coast.

Rio jana mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambapo chama analoshabikia Nigeria liliibuka na ushindi mbele ya Afrika kusini aliweka post kwenye mtandao wake wa kijamii wa X akiwa ameshikilia jezi ya timu ya taifa ya Nigeria na kuweka maandishi yenye bendera ya taifa hilo kuonyesha kuiunga mkono.

Hata hivyo mmoja kati ya mashabiki alijitokeza na kutoa maoni kuwa kwanini huwa anajitokeza baada ya timu hiyo kushinda lakini Rio akachapisha tena picha mbalimbali akiwa Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live