Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki KMC afanyiwa upasuaji

Beki KMC Beki wa kushoto wa KMC, Hance Masoud

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kushoto wa KMC, Hance Masoud hatakuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza mechi zilizobaki za Ligi Kuu kwani amefanyiwa upasuaji wa goti.

Masoud alikuwa miongoni mwa nyota saba wa kikosi cha kwanza waliokuwa majeruhi ambapo sita wamerejea kikosini akiwemo Matheo Anthony na Waziri Junior.

Akizungumza Afisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula alisema tatizo la Masoud litachukuwa muda mrefu kupona tofauti na wenzake, hivyo watakosa huduma yake hadi msimu ujao wa ligi.

“Unajua timu yetu ilianza vizuri lakini ilitetereka hapo kati kutokana na wachezaji wengi kupata majeraha tena wote wa kikosi cha kwanza, hatukuwa na namna nyingine ya kufanya ingawa sasa wachezaji sita wamepona na kurejea kikosini.

“Masoud peke yake ndiye hatakuwa kikosini hadi msimu ujao, maana anauguza goti lake baada ya kufanyiwa upasuaji,” alisema Mwakasungula

Kuhusu mwenendo wa timu kwenye ligi ambapo inashika nafasi ya 12, bosi huyo alisema; “Matokeo yanatuumiza vichwa, , tukizembea itakuwa hatari, viongozi na benchi la ufundi tunapambana ili mambo yasiharibike.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live