Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki AS Roma adondoka Uwanjani, Mechi yaahirishwa

Ndickaaaaaaa Beki AS Roma adondoka Uwanjani, Mechi yaahirishwa

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa klabu ya AS Roma, Evan Ndicka raia wa Ivory Coast alianguka uwanjani mnamo dakika ya 72 wakati wa mechi dhidi ya Udinese hali iliyopelekea mchezo huo kuahirishwa huku ubao ukisoma 1-1.

Kwa bahati nzuri, Ndicka alikuwa kwenye fahamu na kujitambua, lakini alitolewa nje ya uwanja kwa tahadhari.

Taarifa kutoka kwa Roma ilisema kwamba Ndicka “Ndicka aliugua ghafla akiwa uwanjani, lakini alikuwa na fahamu.

Madaktari wa klabu hiyo na wahudumu wa dharura waliitwa uwanjani na baada ya mazungumzo na mwamuzi, mechi iliahirishwa.

Uamuzi huo ulitangazwa kwa umati wa watu baada ya takriban dakika 10 za mashauriano kati ya mwamuzi na timu zote mbili, huku mashabiki wote wakimshangilia Ndicka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live