Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya mwamba imefichwa Old Trafford

Rasmus Hojlund EPL Statistics Mshambuliaji, Rasmnus Hojlund

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Mshambuliaji, Rasmnus Hojlund amebaki kucheka tu baada ya kuulizwa kama mkataba wake kwenye kikosi cha Manchester United imechomekwa kipengele kinachotajwa bei halisi anayouzwa mkali huyo.

Straika huyo wa kimataifa wa Denmark, mwenye umri wa miaka 21, sasa amejipata huko Man United.

Akinaswa kwa Pauni 72 milioni kutoka Atalanta kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, straika Hojlund alishindwa kufunga bao katika mechi 14 za kwanza alizocheza kwenye Ligi Kuu England.

Lakini, sasa ameweka kando ukamne huo, akifunga bao kwenye mechi nne mfufulizo zilizopita.

Wakati Hojlund akionekana kutulia na kuanza kutikisa nyavu, mashabiki wa Man United wanaamini wameshapata suluhu ya tatizo lao kwenye safu ya ushambuliaji.

Akizungumza na shabiki wa Man United, Mark Goldbridge, straika Hojlund alisema kitu ambacho anapenda kukifanya kwenye muda wake wa ziada ni kucheza michezo ya kompyuta ya PlayStation.

Goldbridge baadae alisema, kwenye michuano hiyo ya kompyuta kuna wakati alilazimika kumsajili tena Hojlund, kwa sababu aliondoka kwenda Tottenham kutokana na kipengele kilichokuwa kwenye mkataba wake.

Kisha mkali huyo wa YouTube, alitaka kufahamu kama kipengele hicho hakipo kwenye uhalisia, ndipo Hojlund alipojibu kwa kicheko kikubwa, lakini habari njema kwa mashabiki wa Man United ni straika huyo ambaye amekuwa akishabikia pia Man United tangu mdogo, alijibu: “Hapana.”

Kisha, Hojlund, alitaja kikosi chake cha mastaa watano waliowahi kutamba na miamba hiyo ya Old Trafford na timu yake ilikuwa hivi, golini Peter Schmeichel, beki ni Rio Ferdinand, viungo ni Paul Scholes na Ryan Giggs na mshambuliaji ni Cristiano Ronaldo.

Chanzo: Dar24