Erling Haaland ana kifungu cha kutolewa cha paundi milioni 175 ambacho kinatumika tu kwa timu zilizo nje ya Ligi ya Uingereza, ripoti zimedai.
Jarida moja la michezo lilifichua wiki iliyopita kwamba staa huyo wa Manchester City, ambaye ameanza maisha kwa kishindo katika klabu hiyo tangu uhamisho wake wa paundi milioni 51 kutoka Borussia Dortmund, anapokea paundi 865,000 kwa wiki huko Etihad.
The Athletic sasa wameripoti kwamba mkataba wake wa miaka mitano unajumuisha kipengele cha kuachiliwa, ambacho kitawatahadharisha wababe hao wa Ulaya lakini pia kumfanya Mnorway huyo kushindwa kuhamia kwa mpinzani wake wa Ligi Kuu.
Inasemekana kwamba kifungu cha kutolewa cha Haaland cha paundi milioni 175 kinapatikana tu kwa timu zilizo nje ya Ligi Kuu na itaanza msimu wa joto wa 2024. Kifungu hicho kitapungua karibu na mwisho wa mkataba wake ambao unatarajiwa kumalizika msimu wa joto wa 2027.
Kufikia wakati huo, Haaland ambaye tayari amefunga mabao 20 katika mechi 13 alizoichezea City msimu huu, atakuwa na umri wa miaka 27 na anapaswa kuwa katika kiwango cha juu cha maisha yake ya soka.
Kifungu chake cha kuachiliwa kitawatahadharisha wababe wakubwa wa Ulaya ikiwa ni pamoja na Real Madrid, Barcelona, Paris Saint-Germain na Bayern Munich, ambao wote wamehusishwa hapo awali na Haaland, na wangependa kumuongeza katika klabu zao.
Walakini, kwa vilabu kama Manchester United, Chelsea na wengine wa Ligi Kuu, wanaweza kusubiri na kutumaini kwamba Haaland ni mchezaji huru kufikia mwisho wa mkataba wake wa Man City.
Kufikia majira ya joto ya 2024, nyota wa Real Madrid, Karim Benzema atakuwa na umri wa miaka 36, wakati Robert Lewandowski wa Barcelona atakuwa akifikisha umri huo muda mfupi kabla ya msimu wa 2024-2025 kuanza.
Kwa hivyo ingetengeneza wakati mwafaka kwa vilabu kutazama siku zijazo na kuleta majina ya mmoja wa wachezaji nyota wa kweli wa soka kuatika mwisho wa enzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Ingawa kungekuwa na bonasi za ziada na ada za mawakala za kulipa, ambazo zinatarajiwa kuwa katika kiwango sawa na kile ambacho City ilipaswa kulipa msimu huu wa joto.
Wakati City ililipa Dortmund paundi milioni 51, dili zima pamoja na ada za wakala na bonasi inasemekana kuwa takriban paundi milioni 85.