Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beckham miongoni mwa watakaoinunua Man United

David Beckham Ml.jpeg David Beckham

Thu, 24 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti zinaeleza kuwa Mkongwe wa England, David Beckham yuko tayari kufanya mazungumzo na wawekezaji wengine ili kuungana katika kuinunua Klabu ya Manchester United baada ya wamiliki wake wa muda mrefu familia ya Glazers kuamua kuiweka sokoni.

Kwa uwezo wake peke yake nyota huyo hatoweza kuinunua klabu hiyo. Hata hivyo wanunuzi kadhaa wanaweza wakapendelea kuungana naye ili kuongeza nguvu katika mbio hizo za kuinunua United.

Beckham amewahi kuichezea klabu hiyo kwa miaka mingi, ana historia muhimu kwenye soka la England na dunia, uwepo wake kwenye muungano wa wawekezaji utaongeza uzito wenye thamani kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live