Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beckham atoboa siri ya Charlton

Beckham Vs Charlton Beckham atoboa siri ya Charlton

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mkongwe wa soka na mmiliki wa Inter Miami ya Ligi Kuu ya Marekani, David Beckham alikiri asingeichezea Manchester United kama asingesikiliza ushauri wa Sir Bobby Charlton ambaye amefariki dunia wikiendi iliyopita.

Gwiji huyo wa United amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 kutokana na ugonjwa wa utindio wa akili huku salamu za pole zikizidi kuongezeka.

“Alikuwa mtu mwenye roho ya aina yake. Aliheshimika ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Nikirudisha miaka nyuma, Sir Bobby ndio alikuwa sababu ya kujiunga na Man United, Nilipotembelea shule yake ya soka aliuambia ulimwengu watu wanifatilie sana wakati naanza kucheza soka. Namshukuru sana kwa sababu asingekuwa yeye nisingepata nafasi ya kutimiza ndoto yangu. Hivyo mimi na baba yangu tunamshukuru sana,” alisema Beckham

Beckham na Charlton waliwahi kubeba ndoo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati walipokuwa wanakipiga Man United.

Klabu ya Man United ilikuwa ya kwanza kutoa heshima kwa mchezaji huyo mashuhuri ambaye aliwahi kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha England mwaka 1966.

Taarifa ilisema: “Sir Bobby alikuwa shujaa wa mamilioni ya watu, sio Manchester au Uingereza, lakini dunia nzima.”

Sir Bobby anachukuliwa kama mmoja wa wanasoka bora wa muda wote katika historia na atakumbukwa kutokana na mambo mazuri aliyofanya enzi za uhai wake. Sir Bobby ndiye Muingereza wa kwanza kushinda tuzo ya Ballon d’Or baada ya kubeba Kombe la Dunia mwaka 1966.

Pia alifunga mabao 249 katika mechi 758 akiwa na Manchester United - akiisaidia kushinda kombe lao la kwanza la Uropa mwaka 1968.

Licha ya kucheza kama kiungo, Sir Bobby alifunga mabao 49 zaidi katika mechi 106 alizoichezea England.

Alitumia karibu maisha yake yote ya uchezaji akiwa Man Utd na alisifika kwa pasi zake na mashuti ya mbali.

Chanzo: Mwanaspoti