Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern yamnyatia Decline Rice

Rice WHU Training Decline Rice

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Bayern Munich wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnasa nyota wa West Ham na timu ya Taifa ya Uingereza Declan Rice.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuhitajika sana msimu ujao wa joto, huku Wagonga nyundo wa London wakijiandaa kutoa dau la zaidi ya pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji wao huyo.

Vilabu vya Ligi kuu ya England, Chelsea, Manchester City na Liverpool zote zinasemekana kuwania saini yake lakini sasa wanaweza kukabiliana na ushindani mkali kutoka kwa mmoja wa vigogo wa Uropa.

Ripoti kutoka Hispania zinasema kuwa mabingwa wa Bundesliga Bayern wanamwona Rice kama nyongeza ya ubora kwenye safu yao ya kiungo, huku kocha mkuu wa Bayern Julian Nagelsmann akiamini kuwa mchezaji huyo wa Uingereza anaweza kustawi na Joshua Kimmich katikakati ya uwanja.

Yeye si mchezaji wa kwanza mwenye kipaji ndani ya Primia Ligi kuhusishwa na The Bavarians siku za hivi karibuni, na ripoti zinaonyesha wachezaji wawili wa Tottenham Harry Kane na Heung-Min Son wako kwenye rada zao.

Inasemekana kurejea Chelsea ndilo chaguo linalowezekana zaidi kwa kiungo huyo Rice, huku mmiliki Todd Boehly akitaka kujenga kikosi kipya cha kusisimua huko Stamford Bridge.

Jude Bellingham, ambaye ameanza pamoja na Rice katika mechi mbili za kwanza za Kombe la Dunia za Uingereza huko Qatar, pia yuko kwenye orodha ya matamanio ya Blues.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live