Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern yajiwekea rekodi mbaya kwenye historia yake

Uxbp5J1wUuih Uxbp5J1wUuih 6PBYLQRM1rPx Original 1440x1029 Kiungo mshambuliaji wa Bayern, Thomas Muller akimfariji Lewandowski

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Klabu ya Bayern Munich ilikutana na kipigo kizito kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978 baada ya kucharazwa bao 5-0 dhidi ya Borussia Monchegladbach na kuondoshwa raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Ujerumani.

Ni miaka 43 imepita tangu The Bavarians wakutane na kipigo cha tofauti ya mabao matano ambacho walikipokea kutoka kwa Fortuna Dusseldorf cha bao 7-1 katika mchezo wa Bundesilga.

Kipigo kikubwa kilichosalia katika historia ya Bayern ni kile walichokutana nacho dhidi ya Schalke 04 katika Bundesilga mwaka 1976, lakini kichapo cha usiku wa jana ni cha kwanza katika michuano hiyo ambayo wamechukua kombe lake mara 20.

Gladbach iliongoza kwa mabao mawili baada ya dakika mbili lakini wakawa mbele kwa mabao matatu hadi dakika ya 21 ya mchezo.

Kouadio Kone ,Ramy Bensebaini, Jonas Hofmann na Breel Embolo ndio wachezaji wa Gladbach waliofunga katika mchezo huo uliowashangaza wengi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa mabingwa hao wa Ujerumani, Hassan Salihamidzic amesema ameshtushwa na kwa ujumla hawakuwa mchezoni. 

Chanzo: eatv.tv